Jumatano , 6th Jul , 2022

Mkuu wa Mkoa wa Mara Ally Hapi amwagiza OCD Wilaya ya Butiama kumkamata   mkandarasi wa kampuni ya Chabhoke Construction Co.Ltd ya Serengeti  Sylevester Bija  

Mkuu wa Mkoa wa Mara Ally Hapi

Aidha amemuagiza Mkurugenzi kumtaka Mhandisi wa majengo wa Halmashauri ya Butiama kutoa maelezo ya kutosha baada ya kutumia mbao za kenchi zisizo na dawa kuezeka katika  jengo la kitengo cha dharura kwenye Hospitali ya Wilaya ikiwa ni kinyume na maelekezo ya Serikali.

Amebainisha hayo wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa Hospitali hiyo ambapo alikuta mbao zilizotumika katika kuezeka jengo hilo ni mbao ambazo hazijatibiwa na dawa za kuzuia kubunguliwa na wadudu.

"Haiwezekani kukubali kuona  vifaa vyinavyotumika katika ujenzi wa miradi yetu vinatumika ambavyo sio vilivyo katika makubaliano ya mkataba" amesema Hapi

Aidha kwa upande wao viongozi wa halmashauri hiyo walitupia lawama kwa mkandatasi huyo kwa kufanya kazi kwa kiburi na kutokufuata maelekezo anayopewa na viongozi mara kwa mara na kujikuta miradi huo ukichelewa kukamilika.

"Mkandarasi amekuwa akipatiwa maelekezo ya mara kwa mara lakini anakaidi na kufanya kazi hii kwa atakavyo yeye " amesema Peter Wanzagi.

" Tuliweka haya utaratibu wa kutumia daftari katika ujenzi huu lakini huyu mkandarasi amekaidi matumizi ya daftari hilo lakini wakandarasi wenzie wanaojenga jengo la mama na mtoto wanatumia utaratibu huo" amesema Juma Mfanga Mfanga Mkuu Mkoa.