Jumanne , 12th Sep , 2017

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa serikali itaendelea kukata na kuondoa matumizi yasiyo ya lazima ili kuweza kuboresha  huduma za jamii.

Samia Suluhu Hassan

 

Mhe. Samia Suluhu  amesema hayo leo wakati akizindua Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma Awamu ya Tano 2017/18 - 2021/22 .

Mh. Suluhu amesema Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma ni chachu pia ya kuongezeka kwa mafanikio katika kuboresha  Afya, Elimu na Maji, kutengeneza mazingira mazuri ya biashara, kuondoa mianya ya rushwa.

Aidha amehimiza matumizi ya risiti za kieletroniki kwa Idara za Serikali, Taasisi na Wafanyabiashara na kuwataka wananchi kudai risiti kila wanapofanya manunuzi.

Programu hii iliyoanza mwaka 1998 imekuwa na mafanikio makubwa  ambapo katika awamu hii Serikali imetangaza vita kubwa dhidi ya rushwa, itaboresha mifumo ya kifedha, kuongeza uwezo wa wakaguzi wa ndani ikiwa pamoja na kuwapa mafunzo yanayoendana na teknolojia ya wakati huu.