Jumanne , 19th Oct , 2021

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama Tanzania Samson Mwela amesema TEHAMA ni eneo ambalo serikali imeelekeza nguvu kubwa ili kuhakikisha watanzania wananufaika zaidi kwa changamoto mbalimbali zinazowakabili kutatuliwa.

Mwela ameyasema hayo leo kwenye mahojiano na East Africa TV na East Africa Radio, leo Oktoba 19, 2021 kwenye Ukumbi wa Simba uliopo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) ambapo unafanyika Mkutano Mkuu wa Tehama.

"Mh Rais Samia amezungumza mara nyingi sana kwamba TEHAMA ni eneo mojawapo ambalo tukielekeza nguvu sisi kama serikali linaweza kusaidia sana kutatua changamoto zinazowakabili vijana," amesema Mwela.

Tazama video hapo chini