Jumatano , 15th Nov , 2017

Rungu la sheria ya makosa ya mitandaoni leo limemuangukia mtoto wa aliyekuwa mwanasiasa maarufu Tanzania Chacha Wangwe, Bob Chacha Wangwe, kwa kuhukumiwa kwenda jela mwaka mmoja na miezi sita au kulipa faini ya milioni 5.

Hukumu hiyo imetolewa leo na hakimu Huruma Shahidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam, na mshtakiwa kutakiwa kutekeleza moja ya adhabu hizo alizoambiwa.

Bob Chacha Wangwe alikuwa anakabiliwa na makosa ya kimtandao kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa facebook kwamba 'Zanzibar inakandamizwa na Tanzania Bara na kwamba ni koloni lake'.