Jumanne , 21st Nov , 2017

Aliyekuwa Mwekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa chama cha CCM, Bi, Sophia Simba, kwa mara ya kwanza amezungumza baada ya chama kumrudisha kundini.

Akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television, Sophia Simba amesema ni mapema mno kwa yeye kuzungumza zaidi lakini kikubwa anashukuru kwa chama kumrudisha baada ya kuomba radhi.

"Siwezi kuzungumza chochote kwani ni mapema mno kwangu, ila nashukuru Mungu kwa lililotokea", amesema Sophia Simba.

Sophia Simba alivuliwa uanachama wa CCM kutokana na utovu wa nidhamu, lakini leo chama kimeamua kumsamehe na kumrudisha baada ya kuandika barua kadhaa za kuomba radhi, zilizosomwa hadharani na Rais Magufuli.