Alhamisi , 11th Aug , 2022

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mwanza imesema licha ya taasisi hiyo kupambana na rushwa lakini bado vitendo hivyo vimeendelea kujitokeza kwa baadhi ya maeneo

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza Frank Mkilanya

Imeelezwa kuwa katika kipindi cha mwezi wa nne hadi mwezi wa sita mwaka huu jumla ya malalamiko 115 yamepokelewa huku taarifa za rushwa pekee zikiwa ni 86.

Akitoa taarifa ya miezi mitatu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza Frank Mkilanya amesema bado wanawaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa zinazohusu vitendo vya rushwa ili ziweze kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria ya kuzuia na kupamba na rushwa namba 11/2007.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza amesema wamebaini urejeshwaji mdogo wa fedha za mikopo ya halmashauri zinazotolewa kwa makundi ya vijana, wanawake na wenye ulemavu hivyo kushauri kasi iongezeke