Jumanne , 19th Oct , 2021

Mkurugenzi wa Tehama na Mwenyekiti wa Kongamano la Tano la Mkutano Mkuu wa Tehama 2021, Mulembwa Munaku, amesema Tanzania kwasasa imepiga hatua kama taifa kwenye matumizi ya Tehama na jitihada zinaendelea kuhakikisha hatua nzuri zaidi inafikiwa.

Mkurugenzi wa Tehama na Mwenyekiti wa Kongamano la Tano la Mkutano Mkuu wa Tehama 2021, Mulembwa Munaku (kushoto) akihojiwa na Irene Tillya.

Munaku ameyasema hayo leo Oktoba 19, 2021 kwenye mahojiano maalumu na East Africa TV na East Africa Radio kueleka Mkutano Mkuu wa Tehama, ambapo amekaribisha wadau wajitokeze kwani kutakuwa na fursa nyingi.

''Tumepiga hatua kama taifa kwenye matumizi ya Tehama na ndio maana mtu anaweza kununua umeme akiwa nyumbani lakini bado hatujafika mwisho ndio tunaelekea huko ndio maana tunakaribisha wawekezaji zaidi kwenye Tehama,'' amesema Mkurugenzi wa Tehama, Mulembwa Munaku.

''Tunahitaji wawekezaji wa vyuo vya Tehama nchini ili kuweza kuendelea kutengeneza wabobezi wa Tehama na kama ambavyo Rais Samia amesema tunakwenda kuwa na chuo kikubwa zaidi Afrika Mashariki,'' - ameongeza Mkurugenzi wa Tehama, Mulembwa Munaku.

Aidha amesema kuwa, ''Kesho Jumatano tutakuwa na mjadala jinsi gani ya kufanya uwekezaji ili tuwe na taifa la kidijitali kwasababu yapo mambo ya msingi ya kufanya ikiwemo kutatua changamoto ya mahitaji ya kitehama ikiwemo mifumo na vifaa''.

Tazama video hapo chini