Jumatatu , 23rd Oct , 2017

Serikali ya Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania imetangaza tenda ya kununua Meli itakayokuwa inafanya safari zake kwenye ziwa Victoria kati ya Miji ya Bukoba na Mwanza.

Hilo limebainishwa leo na Rais John Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam, wakati akitoa hotuba baada ya kuwatunuku vyeti wajumbe wa kamati ya Madini iliyofanikisha uchunguzi wa Mchanga wa madini (Makinikia) pamoja na mikataba ya madini kati ya serikali na kampuni ya Barrick.

“Fedha zipo nyingi ndio maana tunaweza kuanzisha miradi mbalimbali na sasa tumetangaza tenda ya kununua na kujenga Meli mpya itakayokuwa inafanya kazi ziwa Victoria kwasababu hakuna Meli tangu ndugu zetu wapoteze uhai kwenye ajali ya MV Bukoba”, amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais ameongeza kuwa tayari nchi ya Korea ya Kusini imeshaonesha nia ya kuchukua Tenda hiyo ya kununua na kujenga Meli itakayokuwa inatoa huduma ndani ya ziwa Victoria.