Jumatano , 18th Jan , 2017

Mfanyabiashara na 'motivation spekear' Eric Shingongo amefunguka na kutoa darasa kwa baadhi ya watu ambao wamekuwa wakifanya vitu nje ya uwezo wao ili tu kutaka kujionesha kwa watu kuwa na wao wanaweza au wana uwezo huo.

Eric Shigongo

Eric Shingongo amewasahi watu kutunza fedha na kufanya matumizi vizuri na kile wanachokitunza wasikae nacho tu ndani bali wanatakiwa kukiwekeza ili kiweze kuzalisha zaidi kuliko kukaa tu ndani.

"Mimi ni mfanyabiashara, hakuna kitu ninachokiangalia kama kubana matumizi yangu. Siwezi kununua kitu kwa milioni tano na wakati kuna uwezekano wa kukipata kwa milioni mbili tena kikiwa na ubora uleule. Kadri siku zinavyokwenda mbele, nabadilisha maisha yangu, sipendi kurundika vitu vingi vya bei kubwa, labda mwingine angeona fahari kumiliki nguo za bei mbaya, kwangu, siwezi kuishi maisha hayo". Alisema Eric Shingongo 

Shingongo anaendelea kusema kuwa hata kama una pesa kiasi gani kumbuka kubana matumizi ya fedha na unapaswa kufanya manunuzi kutokana na uwezo wako.

"Fanya manunuzi kutegemea na uwezo wako usifanye mambo ili uonekane! Tunza fedha hali ni mbaya, unayoitunza iwekeze. Ndugu yangu bana matumizi yako ya fedha na fanya manunuzi ya kawaida hata kama una fedha kiasi gani" alisisitiza Eric Shingongo