Alhamisi , 22nd Sep , 2022

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, amekutana na viongozi wa nchi za Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo  kutokana na msigano unaoendelea baina yao juu matukio ya  kihaini ambayo DRC inasema kwamba Rwanda inayaunga mkono. 

Viongozi hao watatu wamekutana siku ya jana ambapo wote wapo kwenye mkutano wa baraza kuu la umoja wa mataifa huko jijini  New York.

Kwa mujibu wa Rais Macron viongozi hao wanataka kumaliza tofauti zao ikiwemo kukomesha vitendo vya waasi. 

 Waasi wa kundi la M23 wamekua wakitawala eneo la Kaskazini mwa Congo toka mwezi juni. 

 Katika Mkutano huo ambao Rais Félix Tshisekedi  wa Congo  aliilaumu Rwanda kwa kuunga mkono waasi wa M23, Rais wa Rwanda alijibu ka kusema kwamba ‘’lawama haziwezi kuleta suluhu’’