Alhamisi , 25th Aug , 2016

Shirika la Kazi Duniani ILO linakadiria kuwa ukosefu wa ajira kwa vijana kimataifa utafikia asilimia 13.1 mwaka huu wa 2016 na kusalia katika kiwango hicho hadi mwaka 2017.

Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini mkoani Dodoma, Mhe. Antony Peter Mavunde.

Ripoti mpya ya ILO ya mtazamo wa kimataifa wa ajira na kijamii 2016 ikiwalenga hasa vijana, inaonesha kwamba idadi ya vijana wasiokuwa na ajira itaongezeka kwa nusu milioni mwaka huu na kufikia milioni 71 kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitatu kushuhudia ongezeko hilo.

ILO inasema cha kusikitisha zaidi ni idadi ya vijana hasa katika nchi zinazoendelea ambao wanaishi katika hali ya umasikini ama wa wastani au wa kupindukia licha ya kuwa wanafanya kazi.

Takwimu zinaonesha kuwa vijana milioni 156 asilimia asilimia 33.7 wanaofanya kazi wako katika hali ya umasikini ama wa wastani au wa kupindukia ikilinganishwa na asilimia 26 ya watu wazima wanaofanya kazi.