Jumatatu , 28th Jul , 2014

Mkutano wa Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika umemaliza Mwishoni mwa wikii hii jijini Arusha huku swala la unyanyasaji wa kijinsia na elimu kwa mtoto wa kike vimelezwa kuwa tatizo katika nchi nyingi za umoja huo.

Makamu mwenyekiti wa Umoja wa wabunge wanawake wa nchi za Jumuiya ya madola kanda ya kaskazini, Beatrice Shelukindo.

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wa 45 wamesema pamoja na kuwa nchi nyingi zimepiga hatua katika kufikia malengo ya millennia, bado Afrika inakabiliwa na vikwazo kadhaa vinavyo kwamisha mtoto wa kike kupata elimu sawa na mtoto wa kiume.

Makamu mwenyekiti wa Umoja wa wabunge wanawake wa nchi za Jumuiya ya Madola kanda ya kaskazini, Beatrice Shelukindo, amesema kumekuwa na vitendo vya kikatili kwa nchi nyingi kutokana na sera na sheria nyingi kutofautiana lakini vitendo hivyo havitakiwi kufumbiwa macho.

Wakati huo huo, Watanzania wanaofanya kazi kwenye makampuni ya kigeni wametakiwa kuonesha uaminifu pamoja na juhudi ya kazi ili kuvutia idadi kubwa ya wawekezaji kuja kuwekeza nchini.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene amesema hayo jana jijini Dar es Salaam na kufafanua kuwa hatua hiyo itaendeleza sifa nzuri ya Tanzania kuwa ni nchi yenye mazingira mazuri ya uwekezaji katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri Mbene, kwa miaka mingi kumekuwa na sifa mbaya kwamba Watanzania hawana nidhamu ya kazi, hawaamini kiasi cha kuwapa wawekezaji sababu ya kuajiri wafanyakazi wengi wa kigeni na Watanzania kubaki wakihangaika kutafuta ajira.