Jumamosi , 19th Sep , 2020

Mgombea wa Urais wa Chama cha United Peoples Democratic Party, (UPDP) Twalib Ibrahim Kadege amezindua rasmi kampeni za urais za chama hicho huku akisema siku za mwanzo endapo watachaguliwa  wataanza kupambana na rushwa.

Kulia ni mgombea urais wa chama cha UPDP Twalib Kadege na kulia ni mgombea mwenza Ramadhani Ali Abdallah

Akiwa anawahautubia wananchi hii leo, Septemba 19, katika wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi ameweka wazi kuwa ilani ya chama chao inaeleza jinsi ya kupambana na rushwa huku kauli mbiu ya chama hicho ikiwa ni mperampera spidi.

"Mimi ilani yangu inasema Mperampera spidi narudia chama chetu kinasema kipaumbele chake mperampera spidi, sisi UPDP, mkituchagua tu tukikaa ikulu kazi ya kwanza kabisa ndugu zangu nikupambana na wala rushwa kwa sababu rushwa ni adui wa haki" alisema Twalib Kadege.

Aliendelea kufafanua kwa wananchi wa Kilwa,"Haya yote tunayo yalalamikia yanatokana na radhi ya rushwa, nchi yeyote duniani ikiwa na rushwa wananchi wake wanadhoofika, hawajiamani , hawajieliwi kwasababu ya rushwa hii ndio kero kubwa sana" alisema Twalib Kadege