Miongoni mwa wageni 3,000 wakiwemo viongozi mbalimbali wa serikali, ndugu jamaa na marafiki waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa.
Vijana waliopoteza maisha wana umri wa kati ya miaka 13-17 .
Hakuna taarifa rasmi za chanzo sahihi cha vifo vya vijana hao 21, ambao walifariki dunia wakati wakisherehekea kumaliza mitihani yao ya mwisho kwenye klabu hiyo ya usiku.
Wafuatiliaji wa mambo nchini humo wanasema kuwa huenda vijana hao walikosa hewa ama kuvuta hewa chafu yenye sumu ambayo huenda ilisababisha vifo vyao, lakini mpaka sasa hakuna taarifa rasmi.
Janga hilo limeibua upya maswali kuhusu uwepo wa klabu za usiku nchini humo, ikiwemo kuanza kufuatilia leseni na vibali mbalimbali vya uwepo wa maeneo hayo ya burudani., huku vilabu vya usiku kwenye maeneo hayo vikifungwa kufuatia tukio hilo.