Jumanne , 19th Oct , 2021

Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Simiyu, wametakiwa kila mmoja kulima ekari moja ya shamba darasa la zao la pamba, ili kufikia lengo la mkoa huo la kukusanya tani laki tano ya zao hilo la kiuchumi.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohamed Seif Farai

Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohamed Seif Farai, alipozungimza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho katika wilaya ya Itilima mkoani humo.

Amesema ingawa lengo la nchi ni kukusanya tani milioni moja ya zao la pamba, lakini Simiyu lazima iwe kinara katika makusanyo ya zao hilo la kiuchumi.