Jumatano , 1st Jun , 2016

Wabunge waliosimamishwa bungeni kutokana na makosa mbalimbali wamesema kuwa hatua iliyochukuliwa dhidi yao wana wasawasi kuwa bunge hilo litakuwa kibogoyo na litashindwa kufanya kazi yake kama inavyotakiwa.

Bungeni Dodoma

Wakiongea kwa nyakati tofauti Mjini Dodoma, Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Zuberi Kabwe amesema kuwa ni dhahiri wasiwasi waliokuwa nao toka awali unajidhihirisha wazi kuwa bunge hilo litakua ni kibogoyo na kukosa maamuzi.

Nae Mbunge wa Bunda Mhe. Esther Bulaya amesema lengo kuu la adhabu iliyotolewa dhidi yao ni kutaka kupunguza nguvu ya upinzani bungeni pamoja na kutaka kuwatisha wabunge washindwe kuwawakilisha wananchi wao ipasavyo.

Kwa upande wake Mbunge aliesimamisha kwa vikao Kumi mfululizo Mhe. John Heche amesema hata kama atarejea ndani ya bunge hilo ataendelea na misimamo yake ya kutetea wananchi bila woga kwa kujali maslahi ya taifa.

Hati hivyo Baraza la Vijana la Chama cha Demkorasia na Maendeleo CHADEMA wamelalamikia kitendo hicho huku wakimtaka Naibu Spika Mhe. Tulia Ackson ajipime mwenye kama anafaa kuendelea kuliongoza bunge hilo huku Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC),Hellen Kijo Bisimba akisema hatua hiyo imewanyima haki wananchi kwa wabunge waliowachagua.

Sauti ya Wabunge Zitto Kabwe, Esther Bulaya na John Heche wakizungumzia sakata hilo