Alhamisi , 27th Oct , 2016

Wafanyabiashara wa nchi za umojan wa ulaya (EUBG) wamezindua ripoti inayotoa mwongozo kwa Tanzania ya namna ambavyo uwekezaji katika viwanda kwa nchi hizo utakavyoinufaisha nchi na kukuza maendeleo ya viwanda.

 

Akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo, Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa nchi za Ulaya Bwana Mortan Juul amesema EUBG wataendelea kuwekeza Tanzania kwa miaka mingine 5 katika sekta ya madini, mafuta na gesi, utalii, nishati ya umeme, kilimo, TEHAMA, biashara na miundombinu.

Ripoti hiyo inaonesha kuwa kwa mwaka jana pekee nchi za Ulaya ziliwekeza kiasi cha Dola za Marekani bilioni mbili, ambapo katika viwanda wamewekeza kwa asilimia 68 ambapo ulipaji kodi wa makampuni yao makubwa inaonesha kuwa wameongeza mapato ya ndani.

Godfrey Simbeye

Naye  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta binafsi nchini, Bwana Godfrey Simbeye anasema ni vyema serikali ikaboresha sera na kuweka mazingira mazuri ili kuvutia wawekezaji ambao wataongeza kipato na kukuza soko la ajira nchini.