Jumanne , 20th Jun , 2017

Changamoto ya uchache wa Wakilimani wa Lugha ya alama nchini, kutafsiri kwenye vyombo vya habari hasa televisheni umefanya serikali na taasisi nyingine za habari kushindwa kutizimiza lengo la upashaji wa habari kwa watu wote hususani viziwi.

Akizungumza leo Bungeni, Dodoma, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura amesema kuwa takwimu zilizopo kwa nchi nzima kuna wakalimani wa lugha ya alama 70 tu na kati ya hao 15 ndio wenye uwezo wa kufanya kazi kwenye vyombo vya habari.

Bi. Wambura amesema kuwa ili kukabiliana na Changamoto hiyo serikali imetoa jukumu kwa VETA pamoja na Chama Cha Viziwi Tanzania, (CHAVITA), kutoa mafunzo kwa wakalimani waliobaki ili waweze kukidhi vigezo vya utoaji huduma kwenye vyombo vya habari hasa televisheni.