Jumamosi , 24th Oct , 2020

Mtaalam wa masuala ya lishe kutoka Jukwaa la lishe Tanzania (PANITA) Jane Msagati, amewashauri wanaopenda kula chapati na maini na kisha wakashushia soda au chai ya rangi, waache ulaji wa mtindo huo na badala yake washushie juice ya matunda ili kusaidia mwili kuzalisha damu ya kutosha.

Chapati na maini

Ushauri huo ameutoa hii leo Oktoba 24, 2020, wakati akizungumzxa kwenye kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio  na kusema kuwa mtu anapokula hivyo unauwekea uzito mwili wake kuwa na uwezo wa kufyonza virutubishi.

"Mara nyingi tuepuke kula vyakula vyenye viurutubishi vya madini chuma ambavyo vinasaidia katika uzalishaji wa damu mwilini na vitu kama soda na chai ambavyo mara nyingi huzuia ufyonzaji wa virutubishi katika mwilini, hali inayopelekea miili yetu kuwa na upungufu wa hivyo virutubishi", amesema Jane.

Aidha ameongeza kuwa, "Mtu anapokula chapati na maini, ashushie na juice iliyotengenezwa na matunda na maji yaliyo salama kwa sababu matunda ni vyanzo vizuri vya vitamin C, unausaidia sana mwili kuzalisha damu ya kutosha kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya mwili wa mwanadamu".