Jumatano , 18th Jan , 2017

Muungano wa  klabu za waandishi wa habari nchini  UTPC Kwa kushirikiana na wadau wa habari  wamefungua  kesi kwenye mahakama kuu kanda ya Mwanza kupinga sheria mpya ya huduma za vyombo vya habari ya mwaka 2016

Wanahabari wakiwa kazini

Wadau hao wanadai kuwa sheria hiyo imekiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 18 inayotoa haki na uhuru wa mtu kutoa na kupata taarifa.

Akizungumza kutoka katika mahakama hiyo mwanasheria Jebra Kambole amesema katika kesi hiyo ya kikatiba namba mbili ya mwaka 2017 inayosimamiwa na wanasheria 6 wakujitegemea imelenga kuishinikiza serikali kufanya marekebisho ya baadhi ya vifungu kwenye sheria hiyo kikiwepo kifungu namba 8,35 hadi 39 na 52 hadi 59  vya sheria ya huduma za vyombo vya habari namba 12 ya mwaka 2016.

 Kesi hiyo inafunguliwa ikiwa ni siku chache tangu wadau wengine wafungue kesi  kwenye mahakama ya Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam huku wadau wa habari wakiendelea kutilia mgomo kushiriki mchakato wa kutunga kanuni za sheria hiyo.

Wasikilize hapa

  1. Jebra Kambole - Mwanasheria
  2. Jane Mihanji - Makamu wa Rais UTPC
  3. Abubakar Karsan - Mkurugenzi Mtendaji UTPC

 

 

 

Jebra Kambole - Mwanasheria
Jane Mihanji - Makamu wa Rais UTPC
Abubakar Karsan - Mkurugenzi Mtendaji UTPC