Alhamisi , 17th Apr , 2014

Migogoro mingi ya ardhi nchini Tanzania imedaiwa kusababishwa na wanasiasa ambao huchochea wananchi kwa faida na malengo yao ya kisiasa.

Mkuu wa wilaya ya Korogwe mkoa wa Tanga nchini Tanzania Mrisho Gambo

Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo amesema hayo katika mahojiano na East Africa Radio na kwamba wanasiasa hao pia wamekuwa wakihusika na maamuzi mabovu yanayopelekea migogoro ya ardhi.

Mkuu huyo wa wilaya ameongeza kuwa uongozi wake utahakikisha unashughulikia migogoro yote ya ardhi wilayani Korogwe pamoja na kuzuia kutokea kwa migogoro mipya.