Jumamosi , 22nd Oct , 2016

Serikali imewaonya wafugaji waishio kandokando ya hifadhi ya Serengeti kuacha mara moja kuingiza mifugo yao ndani ya hifadhi hiyo kwaajili ya kuchunga kwani maeneo hayo yametengwa kwaajili ya wanyama pori pekee na siyo kwa mifugo

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ,Mhandisi Ramo Makani.

Akizungumza na wafugaji na wananchi wa Kijiji cha Kijereshi kinachopakana na Pori la Akiba la Kijereshi wilayani Busega Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ,Mhandisi Ramo Makani amesema hifadhi za taifa hapa nchini hazina budi kulindwa na kutunzwa ili vizazi vijavyo viweze kuzifaidi.

Amesema baadhi ya wafugaji wa kijiji hicho na kijiji cha jirani wamekuwa wakiingiza mifugo yao katika pori hilo na katika hifadhi ya Serengeti nyakati za usiku na wanapokamatwa na askari huwapigia yowe na wengine hudai kuruhusiwa na viongozi wa kisiasa kuchunga huko.

Kwa upande wao wafugaji wa kijiji hicho wamesema eneo la Pori la Akiba la Kijereshi ni mali yao na kwamba kuna makaburi ya babu zao lakini wanashangaa serikali kulichukua na kwamba hawana maeneo ya kuchungia huku wengi wakikiri kuchungia mifugo yao maeneo ya hifadhini.