Ijumaa , 18th Sep , 2020

Mahakama Kuu ya Tanzania, kanda ya Dar es Salaam, imewahukumu kunyongwa hadi kufa watu watano baada ya kutiwa hatia kwa makosa ya kumuua aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, DkT.Sengondo Mvungi.

Waliohukumiwa ni Msigwa Matonya, Mianda Saluwa, Paulo Mdonondo, Longishu Losingo na John Mayunga.

Pia Mahakama hiyo imemuachia huru Juma Kanungu baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.

Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Seif Kulita, ambapo upande wa mashtaka uliwakilishwa na mawakili, Credo Rugaju, Lilian Lwetabura, Veronica Mtafya.

Akitoa hukumu hiyo Jaji Kulita, amesema ameridhika  na ushahidi wa upande wa mashtaka, hivyo anawahukumu washtakiwa wote kunyongwa hadi kufa isipokuwa mshtakiwa wa tano ambaye ni Juma Kanungu, ambaye ushahidi wa mashtaka haumkumgusa.

Katika kesi ya msingi washtakiwa kwa pamoja walidaiwa kuwa Novemba 3 mwaka 2013 huko Mbezi Msakuzi Kiswegere walimuua kwa kukusudia Dk.Sengondo Mvungi