Alhamisi , 4th Aug , 2016

Jeshi la polisi mkoani Mbeya linawashikilia watu wawili wakikabiliwa na tuhuma za kusambaza Ujumbe wenye kuashiria kuhatarisha amani ya nchi kupitia mtandao wa simu.

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Dhahiri Kidavashari.

Hatua hiyo pia inayohusishwa na Tukio la Oparesheni Ukuta lililopangwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) lifanyike Septemba mosi mwaka huu licha ya serikali kupinga jambo hilo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Dhahiri Kidavashari,wanaoshikiliwa ni pamoja na mkazi wa kata ya Isanga jijini Mbeya Moses Mwaifunga(28) na Meshaki Mgaya(28)mkazi wa Ileje mkoani Songwe.

Kamanda Kidavashari ameonya wafuasi wa Chadema na wananchi wengine kuepuka kusambaza jumbe zinazoonekana kukiuka miiko na maadili ya Utaifa na pale wanapotumiwa kabla ya kuzituma kwa watu wengine wazifute au kutoa taarifa kwa vyombo vya dola.

Amewataka pia wananchi kuhakikisha wanafuata sheria zilizowekwa na mamlaka huku akisisitiza kuwa hata maandiko matakatibu katika baadhi ya vitabu vya dini yanaeleza kuwa Kila Mamlaka inatoka kwa Mwenyezi Mungu.

Sauti ya Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Dhahiri Kidavashari