Jumanne , 13th Oct , 2015

Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda amefariki dunia jana jioni nchini India alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu ya figo yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.

Dkt. Abdallah Kigoda, aliekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashilila amethibitisha taarifa hizo, na kusema kuwa Dkt Kigoda alikuwa akitibiwa katika hospitali ya Apollo, New Delhi na kwamba taarifa zaidi zitatolewa baadaye.

Kwa mujibu wa kaka wa marehem Sadiki Kigoda aliyezungumza na EATV siku chache zilizopita, alisema kuwa Dkt Kigoda alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya figo kushindwa kufanya kazi.

Taarifa zaidi juu ya msiba huo ikiwa ni pamoja na taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu na mipango yote ya mazishi zitaendelea kutolewa na serikali pamoja na ofsi ya bunge kwa kushirikiana na familia ya marehemu.

Waziri Kigoda anakuwa waziri wa pili kufariki dunia wakati kamepni za uchaguzi mkuu Oktoba 25 zikiendelela huku akiwa ni mgombea wa nne katika nafasi ya ubunge kufariki dunia katika kipindi hiki.