Jumatano , 6th Jul , 2022

Jeshi la zimamoto Mkoani Rukwa kwa kushirikiana na Hifadhi ya msitu wa Mbizi wametoa mafunzo ya kudhibiti na kuzuia majanga ya moto kwa vijana mia moja kutoka katika Kamati ya mazingira ya vijiji kumi vinavyozunguka Hifadhi ya msitu wa mbizi ili kusaidia kutunza mazingira

Awali  Baraka Chelela ambaye ni Kaimu  mhifadhi  wa msitu wa mbizi akiongea katika kufunga  Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa mda wa siku nne kuwa ni pamoja na kuishirikisha jamii katika kulinda mazingira ya misitu huku   Konstable Joston Seme kutoka kitengo cha Elimu na mafunzo kwa Umma kutoka jeshi la zimaoto na uokoaji  akitoa wito kwa wananchi kufatilia mafunzo yanayotolewa na jeshi hilo ili kuepukana na majanga.

Kwa upande wake baadhi  ya vijana walioshiriki mafunzo hayo ya kuthibiti na kuzuia majanga ya moto  yaliyoenda sambamba na zoezi la  kuchoma msitu na kuthibiti moto   wakaeleza manufaa wanayoyapata kupitia msitu wa mbizi.