Jumanne , 20th Jun , 2017

Wizara ya habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetakiwa kufuata Miongozo na sheria za kusimamia vyombo vya Habari na maudhuhi yao ili kuepusha kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari nchini.

Waziri wa Habari,Michezo, Sanaa na Utamaduni, Harrison Mwakyembe.

Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Waharir{TEF} Deudas Balile, amesema kuwa, kitendo cha kulifungia gazeti la Mawio ni kinyume cha sheria hivyo na kwamba ni vyema Wizara ikawa mlezi na kufanya majadiliano na vyombo vya habari ili kuwezesha uhuru wa habari na utawala wa sheria kufuata mkondo wake.

Tamko hili limetolewa ikiwa ni siku chache baada ya serikali kufungia gazeti la MAWIO kwa kile kilicho daiwa kukiuka baadhi ya vifungu vya sheria katika sheria mpya ya huduma za habari ya mwaka 2016 kuwa sio kweli, kwani vifungu vya sheria hiyo vinataka Waziri kupeleka madai Mahakamani ili iamuliwe endapo nikosa kisheria.