Entertainment News
Moja ya mwanamuziki wa Uganda mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni, Lillian Mbabazi ambaye alikuwa ni moja ya wanadada wanaounda kundi la Blu 3 amefahamika kuwa ni mjamzito kwa mara nyingine tena.
Lilian ambaye anaaminika kuwa na ujauzito wa miezi miwili sasa, tayari ana mtoto wa miezi 8 ambaye baba yake ni yule yule mkali Moze Radio kutoka Goodlyf crew.
Lilian na Radio walikutana na kuanza mahusiano mwaka 2009 wakati walipokuwa wanarekodi ngoma ya “Where You Are” iliyokamata chati vilivyo katika kipindi hicho.
Print
More Entertainment News
Prime Time
EATV Shows