Ijumaa , 4th Dec , 2020

Mdogo wa msanii Alikiba kutoka Kings Music Records,  Abdu Kiba amevunja ukimya kwa kile kinachoendelea mitandaoni kuhusu video ya Nandy na Alikiba kwamba imesababisha sintofahamu kwenye ndoa ya kaka yake huyo na shemeji yake Aileenalora.

Msanii Alikiba na mkewe upande wa kushoto, kulia ni Abdukiba

Akijibu kuhusiana na hilo baada ya kusambaa kwa maneno kuhusu matendo ya video hizo za nyuma ya kamera katika wimbo wa nibakishie ya Nandy ft Alikiba, Abdukiba amesema kuwa 

"Siwezi kujibu suala la Ali na mke wake kwa sababu silali nao hivyo sijajua kuna nini, ila kwenye familia hakuna tatizo kwa sababu wanajua sisi ni wanamuziki pia tushapata idhini kutoka kwa Mama ingawa kunaonekana na kuhisiwa kuna matendo tofauti, kazi za mitandaoni hatuwezi kuzijaji na huwezi kumpangia mtu akujibu nini" amejibu Abdu Kiba 

Zaidi tazama majibu kamili hapa chini kwenye video.