Aby Dad ampigia magoti Ommy Dimpoz

Friday , 14th Jul , 2017

Prodyuza Aby Dad amefunguka mbele ya kamera na kumtaka radhi msanii Ommy Dimpoz kwa kumshutumu kuiba wimbo wa 'Cheche' ambao ni wa msanii wake kitu ambacho amegundua siyo kweli.

Prodyuza Aby Dad

 Abydad ameomba msamaha huo kwa Ommy huku akidai kwamba hakutumia busara kuongelea jambo hilo kwenye mtandao wa kijamii na vyombo vya habari.

"Mimi ni binadamu, nachoweza kusema ni Ommy anisamehe kwani ni hasira ndizo zilizofanya nishindwe kumtafuta 'direct' nikatumia mitadao ya kijamii. lakini pia mwanzo sikujua kama yeye alikuwa anatambua au la kama kazi hii imeibiwa na baada ya kujua hilo nimeshatambua makosa, brother anisamehe kwa hili", alisema.

Msanii wa Ommy Dimpoz

Akimzungumzia Mtunzi Goodluck Gozbert (Lollipop), Aby Dad amesema kwamba hawezi kumtafuta na kuzungumza naye kwani anajua amefanya dhambi ya makusudi kuchukua kitu kisichokuwa chake.

"Wahusika waliompatia Ommy wimbo sijawatafuta kwani wanajijua wamefanya dhambi ya makusudi, hasa Lollipop ambaye alisema anataka kumsaidia mdogo wetu mwisho wa siku amefanya dharau. Lakini bado naendelea kumshangaa kwa kitendo alichokifanya" Abydad aliongeza. 

Hivi karibuni Aby Dad alitoa tuhuma akizielekeza kwa msanii Ommy Dimpoz, Lollipop pamoja na Kidbway kuwa wamemuibia wimbo wa msanii wake ambaye aliuandaa tangu Januari mwaka jana, ambapo amedai alimkabidhi Lollipop 'beat' na 'verse' moja baada ya hapo alishtuka kuusikia wimbo huo akiwa unatambulishwa na msanii Ommy kuwa ni wake.

Recent Posts