Jumamosi , 16th Oct , 2021

Msanii wa hip hop Bongo, Chidi Beenz anatarajia kuachia album yake mpya hivi karibuni baada ya kuachia orodha ya nyimbo 18 ambazo zinazounda mseto mzima wa album hiyo mpya iliyopewa jina la “Wa2 Wangu”.

Picha ya pamoja msanii Chidi Beenz na Baddest 47

Chidi hajaweka wazi tarehe rasmi ya kuachia album hiyo ambayo itakuwa na collabo za wasanii kutoka Tanzania na nje kama Badest 47, Only1pabo, Brian Simba na Scar Mkadinali kutokea nchini Kenya.