Mchekeshaji Mkali Wenu upande wa kushoto, kulia ni Alikiba
"Kitu chochote kinaweza kutokea, kama menejmenti yangu ikisema nifanye kazi na Alikiba nitafanya naye, kwa sababu Alikiba ni mshkaji wangu na namuandikia nyimbo, hata hii nyimbo aliyotoa ya mediocre nilikuwa nayo muda mrefu aliniomba nikamuandikia, ukiangalia ina utofauti na nyimbo zake zingine" amesema Mkali Wenu
"Kumuandikia mtu haimaanishi kama hauna sauti ila Alikiba yeye ana sauti nzuri, mimi nina sauti ila sio nzuri kwenye kuimba, nyimbo ya mediocre imekaa vizuri kwake nilishawahi kumpa Nay wa Mitego akasema haiwezi kuiimba".
Aidha Mkali Wenu amesema 'role model' wake alikuwa ni marehemu Sharo Milionea ambaye alianzia kwenye uchekeshaji kisha kuimba hivyo wasishangae kumuona na yeye akianza kuimba.
Zaidi tazama hapa chini kwenye video.