Alikiba ampagawisha Waziri Nape Nnauye

Friday , 17th Feb , 2017

Msanii Alikiba ambaye leo ameachia remix ya wimbo wake wa 'Aje' ameonesha kumkosha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye kiasi cha Waziri huyo kusema kuwa Alikiba ni kati ya wasanii wanaofanya ajisikie fahari kuwa Waziri

Nape (Kushoto), Kiba (Kulia)

Mhe. Nape Nnauye amesema hayo leo baada ya msanii huyo kukabidhiwa tuzo yake katika kituo kimoja cha Television nchini Afrika Kusini na kuachia kazi yake mpya ambayo imeonesha kuwakosha watu wengi. 

"Kiba! Big Up! Am so proud of you! we ni mmoja wa wasanii wanaonifanya nijisikie fahari kuwa Waziri wa Sanaa Tanzania! May allah bless you!" aliandika Nape Nnauye 

Msanii Alikiba ni kati ya wasanii wachache kutoka Tanzania ambao wanaiwakilisha vyema nchi kupitia muziki wao. 

 

Recent Posts

Msanii Z Anto

Entertainment
Level yangu Alikiba na Diamond - Z Anto

Msanii Chid Benzi akiwa katika studio za Friday Night Live.

Entertainment
Chid Benz amkana Babu Tale

Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali.

Sport
Mzee Akilimali azidi kumchana Niyonzima

Mchezaji Victor Wanyama

Sport
Wanyama amtabiria makubwa Samatta