Jumatano , 29th Jun , 2022

Baby Dady wa Ruby na Aunty Ezekiel Kusah amesema asilimia 80 ya mashabiki zake ni wanawake japo ajawasahau mashabiki zake wa kiume.

Picha ya msanii Kusah

"Kwenye mwanamke mbele nyuma yake kuna mwanaume, mziki wangu mkubwa mashabiki wangu ni watoto wa kike, sijalenga kitu kibaya ila ladies is first"

"Katika takwimu za platform zangu asilimia 80 wanaonisapoti ni wanawake kwa hiyo lazima niwape sifa yao japo wanaume pia ni wanangu".

Kusah amesema hayo kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio ambayo inasikika kila siku ya J3 mpaka Ijumaa saa 7:00 mchana mpaka 10:00 jioni.