Jumapili , 20th Aug , 2017

Msanii wa muziki wa bongo fleva Juma Kassim maarufu kama Juma Nature, ameweka wazi mipango yake ya kuingia kwenye siasa, na kusema kuwa akifikia uamuzi huo ana imani hatofeli kwani jamii yake inamkubali kwa asilimia mia.

Msanii Juma Nature

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio, Juma Nature amesema kwa jinsi alivyojiwekea msingi imara katika eneo lake, ana imani bila kujali ni chama gani atatumia kugombea, lakini lazima atafanikiwa kuingia mjengoni kuwawakilisha wananchi wake, huku akiwapindua wale waliozoeleka kuingia bungeni.

Msikilize hapa chini..