Jumamosi , 28th Nov , 2020

Msanii wa filamu hapa nchini Aunty Ezekiel amejifungua salama mtoto wa kiume ambapo kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram ameweka taarifa hiyo kwa kuandika kuwa "Asante mungu kwa hii zawadi".

Msanii wa filamu Aunty Ezekiel

Sasa hizi hapa ni comments za mastaa wenziye ambao wamempongeza baada ya kuweka ujumbe huo kwamba amejifungua.

"Unajishaua jamani uwiii, hongera baby" Wema Sepetu 

"Hongera my love" Elizabeth Michael 

"Nawapenda sana" Nandy 

"Hongera sana boss wangu, ila chonde chonde kama ni wa kiume usije ukarogwa ukampa jina la Idris" Billnass

"Hongera sana mama wawili, jitahidi unifikie basi" Monalisa 

Huyo ni mtoto wa pili wa Aunty Ezekiel japo bado haijafahamika rasmi ni nani baba halali wa mtoto huyo, mtoto wake wa kwanza ni wa kike anafahamika kwa jina la Cookie ambaye amempata na mzazi mwenzake Mose Iyobo.