Jumanne , 21st Feb , 2017

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepanga mwaka huu kutoa tuzo kwa shule mbalimbali nchini ambazo zinafundisha masomo ya sanaa katika shule hizo ili kuwapa hamasa.

Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza amezungumzia jambo hilo kwenye kipindi cha Planet Bongo na kusema wana mpango wa kutoa tuzo hizo kwa shule ili kujenga ushawishi kwa shule mbalimbali ziweze kutoa masomo ya sanaa kwa sababu mihutasari (sylabus) ya masomo hayo zipo.

"Tunajenga ushawishi masomo ya sanaa yaanze kufundishwa mashuleni sababu sylabus za masomo hayo zipo, tunataka mwisho wa siku mtu awe msanii aliyesomea sanaa, na tutatoa tuzo kwa mwaka huu wa fedha kwa shule za sekondari ambazo zinafundisha sanaa siyo sanaa katika ile dhana ya sanaa 'Arts' lakini sanaa ile ya 'fine arts', sanaa za maonesho na muziki, tutatoa tuzo kwa shule hizo kuwaonesha kwamba hamjakosea njia mpo mahali sahihi" alisema Godfrey Mngereza