Jumamosi , 17th Jun , 2017

Msanii wa miondoko ya RnB, Ben Pol anayehit na ngoma ya 'tatu' amesema kwa sasa anapata wakati mgumu sana kujua kesho yake kutokana na mitandao ya kijamii kumuandika mara kwa mara.

Mwanamuziki Ben Pol

Ben anasema imefika wakati hata anapoulizwa au kuelezea jambo kwenye vyombo vya habari anakuwa makini kwa kuhofia kukaa roho juu kwa kuwa hafahamu baada ya hapo watu wa mitandaoni wataamka na taarifa zipi kuhusu yeye.

“Unajua baadhi ya mitandao wanakuuliza jambo fulani,  ukifungua simu utashtuka mwenyewe jinsi wanavyoandika, yaani nakuwa na wakati mgumu sana,” alisema Ben Pol.

Hivi karibuni msanii huyu amekuwa akiandamwa na maneno mengi mitandaoni toka alipopiga picha za 'cover' ya wimbo wake wa tatu akionekana sehemu kubwa ya mwili kuwa tupu.