Jumatano , 11th Jan , 2017

Mwanamuziki Ben Pol anasema kwa mara ya kwanza aliposikilizishwa wimbo wa 'Muziki' wa Darassa aliwaza mambo mawili katika akili yake.

Ben Pol

Jambo la kwanza anasema aliwaza kuwa wimbo ule ulikuwa unahitaji mwimbaji lakini kingine aliona wimbo ule ni 'hit song' hivyo anahitaji kupata lifti kwenye wimbo huo.

Ben Pol alisema hayo jana alipokuwa kwenye kipindi cha Planet Bongo na kusema ilibidi amshawishi Darassa kwa kumwambia kuna sauti anataka kuiweka kwenye wimbo huo ili msanii yoyote akayekuja kuimba apite kwenye njia hizo.

"Nakumbuka tulikuwa Singida na Darassa akanisikilizisha ule wimbo, nilipousikia niliwaza mambo mawili moja niliwaza kuwa wimbo ule ulikuwa unahitaji mwimbaji, lakini niliona ile ngoma ni 'hit song' hivyo nilikuwa nahitaji lifti, nikamwambia Darassa tukirudi mjini naomba nikuwekee sauti kwenye wimbo huo ili mtu yoyote atakayekuja kuimba apite njia hizo, lakini baada ya kuweka sauti yangu baada ya hapo Producers walisema tu nimalize mwenyewe" alisema Ben Pol 

Darassa

Mbali na hilo Ben Pol anasema ameamua saizi kufanya kazi na watu ambao wanaweza kusimamia kazi zao na si wale ambao wanafanya kazi harafu wanaziweka ndani au hawazipi nguvu kazi hizo.

"Saizi nimeamua ni bora nifanye kazi na watu wachache ambao kazi zao watazifanyia kazi siyo kufanya kazi na wasanii 40 harafu watatu tu ndiyo wanazipa nguvu kazi sasa si bora nifanye na watu watatu ambao naona kabisaa watazifanyia kazi ngoma hizo na kuzifikisha mbali zaidi" alisema Ben Pol