Ben Pol ni shujaa - Dogo Janja

Friday , 19th May , 2017

Baada ya msanii Ben Pol kupiga picha zenye ukakasi na kuzipost kwenye ukurasa wake wa Instgram rapa Dogo Janja ameibuka na kusema kuwa kitendo alichokifanya Ben Pol ni kitendo cha kishujaa sana kwani wengi hata yeye asingeweza kufanya jambo hilo.

Dogo Janja amesema hayo leo alipokuwa kwenye kipindi cha 5Selekt na kusema jambo hilo alilofanya Ben Pol linahitaji moyo na kusema inawezekana kwa sasa likawa na faida kwa msanii huyo ila athari ya kitendo hicho atakuja kuiona baadaye.

"Labda brother alijiuliza akivaaje atapendeza akaamua asivae kitu tu mbona freshi, lakini mimi sidhani kama nitaweza kufanya jambo kama lile kuwaonyesha watu 'Too much' hapana aisee, vitu kama vile vinaishi milele. unaweza kufanya leo ukapata maslahi lakini kesho kikawa na athari katika maisha yako" alisema Ben Pol 
 

Recent Posts

Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Wakili Anna Henga.

Current Affairs
LHRC yaipa neno serikali kuhusu mauaji

Rais Magufuli akiwa kazini

Current Affairs
Magufuli ateua Naibu Kamishna Mkuu TRA

Kamishna Simon Sirro

Current Affairs
Kamanda Sirro awajibu waliosusia maiti

DCP Ahmed Msangi, RPM Mwanza

Current Affairs
Binti wa miaka 15 abakwa na vijana wanne