Jumatano , 26th Nov , 2014

Msanii wa muziki anayezipanda chati za muziki kwa kasi hapa Bongo, Cindy Rulz amesema kuwa, tasnia ya muziki hususan wa Rap hapa Tanzania imetawaliwa na mfumo dume kutokana na wanawake wanaorap kudharauliwa na pia kutokupeana sapoti wao kwa wao.

msanii wa muziki wa kurap nchini Cindy Rulz

Rapa Cindy amesema kuwa, mfumo wa game ya rap unaonekana ni wa kiume zaidi, huku kwa upande wa pili ukweli ni kuwa kuna wanawake wenye uwezo wa kurap kuliko hata vile wanavyofanya wanaume.