Jumanne , 19th Aug , 2014

Mashindano makubwa ya kudance Afrika Mashariki, Dance 100% 2014 hatua ya Robo Fainali yanatarajia kutikisa kiburudani siku ya Jumamosi tarehe 23 Agosti mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Mashindano ya kucheza muziki nchini Tanzania Dance 100% 2014

Mashindano haya yatakayohusisha makundi 16 makali ya kudansi, yatafanyika katika uwanja wa Oysterbay Don Bosco, na makundi yataanza kuonesha uwezo mbele ya majaji kuanzia saa 6 mchana.

Tukio hili linatarajiwa kuwa na msisimko wa aina yake hasa kutokana na ushindani na uwezo mkubwa wa makundi yote ambayo yanashiriki. #2014Dance100%.