Alhamisi , 29th Sep , 2016

Msanii wa Bongo Fleva nchini Ruby amesema shindano la Dance100% linaloendeshwa na EATV limeweza kuibua vipaji vya vijana mbalimbali ambao wanauwezo wa kupata kazi katika maendeo mbalimbali nchini.

Ruby

Akizungumza na EATV, Ruby amesema amefurahishwa sana kuona vijana wengi wakijitokeza kushiriki shindano hilo jambo ambalo linaonesha kwamba muamko ndani ya jamii umeongezeka.

“Mimi ni mara ya kwanza kushuhudia LIVE shindano hili lakini kumbe huwa nakosa burudani ya aina yake, vijana wanajituma sana na kupitia shindano hili vipaji vingi vinaibuka na vijana wanatambulika katika maeneo mbalimbali” Amesema Ruby

Fainali ya shindano la Dance100% ambalo limemalizika hivi karibuni itaoneshwa na EATV pekee siku ya Jumapili saa moja jioni ambapo kundi Team Makorokocho liliweza kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 7.

Tags: