Jumanne , 28th Mar , 2017

Mwanamuziki Dayna Nyange mwenye ‘hit song’ ya ‘Komela’amefunguka yake ya moyoni na kusema wasanii wanakufa njaa kutokana na hali ya maisha kuwa ngumu kwa sasa mpaka kupelekea kukosa kufanya matamasha ya kimuziki.

Dayna Nyange

Mrembo huyo amedai kuadimika kwa ‘show’ kumechangia kwa wasanii wote kuwa hali mbaya maana wengi wao wanategemea kuingiza kipato kutumia kazi hiyo huku akiwashauri wenzake wasitegemee sanaa pekee yake.

“Kwenye muziki mambo yamekuwa ‘tight’si kama zamani na siyo kwenye muziki wetu wa bongo fleva, mimi nazungumza na watu wanaofanya mpaka muziki wa dansi nao wanalia njaa hivyo hivyo, mifukoni hakuna kitu na ili kupata chochote mtu inabidi kupambana kweli kweli kutafuta namna ya kupiga show na kutotegemea muziki pekee”. Alisema Nyange

Pamoja na hayo msanii huyo ameeleza pia uchache wa mapromota umechangia kwa kiasi fulani wasanii hao kulalamika njaa kwa kuwa walishazoeshwa kipindi cha miaka ya nyuma kutafutiwa show na watu hao hivyo maisha yao yalikuwa laini.