Jumapili , 27th Jul , 2014

Msanii nyota nchini ambaye nyota yake inazidi kung'ara katika tasnia ya muziki kimataifa, Diamond Platnumz ameshinda tuzo mbili za muziki za AFRIMMA 2014.

wasanii Lady Jaydee na Diamond wa Tanzania

Mkali huyo ameshinda tuzo hizo mbili zikiwemo za Msanii Bora wa Afrika Mashariki na Wimbo Bora wa kushirikiana na wasanii nchini Marekani.

Aidha mwanadada Lady Jaydee aka 'Anaconda' naye ametwaa tuzo ya msanii bora wa kike Afrika Mashariki katika tuzo hizo maarufu za Afrimma 2014 zilizofanyika nchini Marekani.