Gabo kushusha nyingine 'Siyabonga'

Saturday , 15th Jul , 2017

Staa wa filamu nchini Gabo Zigamba, yupo mbioni kuachia kazi mpya inayoitwa ‘Siyabonga’ ambayo imeelezwa ni kali na iliyobeba uhalisia.

Gabo Zigamba

Gabo ambaye anatamba na filamu yake fupi ‘Kisogo’, ambayo ameshirikiana na Wema Sepetu, alisema ujio wa kazi hiyo mpya ni kutekeleza kwa vitendo mpango wake wa kuleta mapinduzi katika tasnia hiyo.

Gabo ni msanii pekee wa kiume anayetazamwa na mashabiki wengi wa filamu za hapa nchini na kuonekana kuwa anaweza kuziba pengo la marehemu Steven Kanumba.
 

Recent Posts