Ijumaa , 21st Jul , 2017

Baada ya kufanyiwa operesheni zaidi ya 10 zilizotokana na tatizo la Endometriosis,  Miss Tanzania 2001 na mwanamitindo wa kimataifa Happiness Magese amejifungua mtoto wa kiume akiwa kilogram 2 na gram 9, Alhamisi ya Julai 13 2117 huko nchini Marekani

Millen aliwahi kujitangaza hadharani kuwa ni muhanga wa  tatizo la 'Endometriosis',  tatizo ambalo huwakuta wanawake wengi pindi wanapoingia kwenye hedhi na kusababisha kuharikibika kwa mimba pia , na tatizo hili liliharibu mimba zake nyingi alizowahi kupata.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mrembo huyo aliandika,

"Mungu nakushukuru kwa kunifanya mwanamke na hatimaye nimekuwa mama, Mungu nakushukuru kwa kunirudishia baba yangu, jina lako lihimidiwe. Nakupenda sana mwanangu, Prince Kairo Michael Magese amezaliwa saa 12 na dakika 58 asubuhi akiwa na uzto wa kilo 2 na gram 9, Julai 13, 2017,”  sehemu ya ujumbe aliouandika  Millen usiku wa kuamkia leo.

Happiness akiwa mjamzito.

Mrembo huyo amefanikiwa kupata mtoto huyo ikiwa na mtu ambaye alishakata tamaa na kuwahi kukiri mwaka jana kwenye chombo kimoja cha habari hapa nchini kwamba anataka kuondokana na maumivu ya kila mwezi kwa kuchagua njia ya kuondoa kizazi.

Tunampongeza sana Hapiness Magese kwa kumpata mtoto Kairo, ikiwa ni pamoja na  kupambana katika kujitoa kwenye kutoa elimu juu ya ugonjwa wa Endometriosis.

Happiness Magese akiwa na mtoto wake mwenye umri wa wiki moja.