Ijumaa , 23rd Jun , 2017

Mkongwe Dudubaya 'Mamba' amewaomba wakongwe wenzake kutowa -diss wasanii wadogo wanaofanya vizuri kwenye game ya sasa , huku akiongeza kama wanahitaji heshima zaidi wanapaswa kujijengea kwanza kabla ya kupatiwa.

Dudubaya akiwa na Professional Dj wa EA radio, Dj Dea ndani ya studio za EA radio.

Dudubaya amefunguka hayo leo kwenye uzinduzi rasmi wa heshima ya bongo fleva ndani ya kipindi cha Planet Bongo na kusema kwamba wasanii wakongwe wanapaswa kujitengenezea brand yao ili waweze kuendelea kuwepo kwenye 'game' huku akiongeza kwamba kama kazi zikifanyika vizuri wanaweza kurudi katika nafasi zao

"Mi ningeomba wasanii wakongwe tuache kuwa-diss hawa watoto wanaofanya vizuri katika game, cha kwanza tutambue siyo lazima kila siku tuonekane sisi tu, ndio maana tunapata watoto wa kuturithi. Lakini utakuta baadhi ya wasanii wakongwe wamekaa pamoja wanakula bangi hata sabini wanalalamikia watoto wanaojitafutia rizki zao, nawaambia mtakufa" , Dudubaya alifunguka.

Kuhusu tamasha la Heshima ya Bongo Fleva

Kipindi cha Planet Bongo chini ya East Africa radio inarudisha heshima kwa wasanii wa bongo Fleva kwa kuandaa tamasha lenye kuhusisha wasanii waliofanya kazi ya muziki miaka ya nyuma kufanikiwa  kuwaamisha watu wengi kwamba muziki ni kazi na siyo uhuni siku ya jumamosi ya julai 1 Dar Live Mbagala.

Tamasha hilo lililopewa jina la Heshima ya Bongo Fleva na kipindi cha planet bongo  litawaweka wasanii wakongwe kibao jukwaa moja ikiwa ni pamoja na kuwakutanisha na mashabiki zao huku muziki na hadithi zote zikiwa ni za zamani ili.

Baadhi ya wasanii watakaokuwepo kwenye orodha ya kupatiwa heshima hiyo ni Mkongwe Dudubaya, Mnyama TID, Z. Anton, Juma Nature, Mabaga Fresh, Mandojo na Domokaya, Solid Ground Family na wengine wengi watapigiwa mizinga ya heshima kwa kutengeneza misingi imara ya muziki.

Heshima ya Bongo fleva itatambua michango mbalimbali iliyofanywa na wasanii hao kwa Kiingilio cha shilingi 7000 za kitanzania huku wimbo ukiimbwa mmoja tu kwamba HESHIMA YA BONGO FLEVA , HIVI NDIO INAFAA KUFANYWA.