Alhamisi , 24th Jul , 2014

Aliyekuwa mwakilishi wa Tanzania katika onesho la kipekee la kusaka vipaji Afrika Mashariki Hisia amesema kuwa kuna umuhimu wa wasanii kijikita zaidi katika muziki wa Live watumbuizapo stejini.

mwanamuziki Hisia wa nchini Tanzania

Hisia ameongezea kusema kuwa muziki wa live unaongeza ladha zaidi katika maonesho ya moja kwa moja ambayo wanayafanya mbele ya mashabiki zao.

Binafasi Hisia kwa sasa amejikita katika hili kama mfano, akiwa ametengeneza maonesho yake yanayokwenda kwa jina la "Muziki wa Hisia", huku akiwaahidi mashabiki wake kazi mpya kabisa kutoka kwake, ambayo ataizindua mwezi ujao na hapa mwenyewe anaelezea kwa kina.