Jumapili , 20th Sep , 2020

Tanzania imejaliwa na vipaji vya watangazaji wengi wazuri kwa sasa, ukiachilia mbali yale majina ya watangazaji pendwa kama Dulla Planet 'Rais wa BongoFleva',Salama Jabir,Sam Misago,Fredrick Bundala,Millard Ayo,Adam Mchomvu au B Dozen.

Mtangazaji wa East Africa TV na East Africa Radio King Smash

Kwa sasa kuna jina moja tu ambalo linaongozwa kutajwa kama ndiyo mtangazaji bora wa kizazi hiki ambaye ni King Smash kutoka kipindi cha The Cruise ya East Africa Radio na eNewz ya East Africa TV.

Kupitia EATV & EA Radio Digital tumepiga stori na mtangazaji huyo ambaye amefunguka kuhusu watu kumtaja kama ndiyo mtangazaji bora kwa sasa.

"Inanipa nguvu kuendelea kufanya zaidi kwa sababu naamini bado sijafanikiwa kufika ambapo nataka ila comments ambazo nazipokea huwa zinanipa moyo wa kufanya vizuri, hata mimi kuna mtu ambaye namfuatilia na kunishawishi kama Dullah Planet ambaye amenifanya kufavya hichi ambacho nakifanya

Zaidi mtazame hapa chini akiyazungumzia hayo.